Ikiwa maneno haya[1] aliambiwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia Mtume, hivyo usishangazwe endapo utawasikia watu wakiwapaka na kuwatuhumu wanachuoni kwamba wako hivi na vile. Shaytwaan huwachochea watu hawa ili wawaponde wanachuoni. Kwa sababu [shaytwaan anajua] wanachuoni wakiangushwa na ikawa watu hawawaamini tena, kutakosekana watu wenye kuwaongoza watu katika Kitabu cha Allaah. Ni nani atayewaongoza watu katika Kitabu cha Allaah ikiwa wanachuoni hawaaminiwi na maneno yao hayasikizwi? Mashaytwaan na pote lake ndio litawaongoza.

Kwa ajili hii ndio maana kuwasengenya wanachuoni ni jambo kubwa kuliko kuwasengenya watu wengine wasiokuwa wanachuoni. Kumsengenya asiyekuwa mwanachuoni ni usengenyaji unayemsibu yule msengenywaji peke yake. Unamdhuru yule yule msengenywaji na yule msengenyaji. Tofauti na wanachuoni kusengenywa. Jambo hilo linaudhuru Uislamu mzima. Kwa sababu wanachuoni ndio ambao wamebeba ujumbe wa Uislamu. Pale ambapo maneno yao yatakiwa hayaaminiwi, basi ujumbe wa Uislamu unaangushwa. Hilo linakuwa na madhara kwa Ummah wa Kiislamu.

Ikiwa kula nyama za watu kwa kuwasengenya ni kula nyama zao ilihali ni maiti [nyamafu], basi [itambulike kuwa] kuwasengenya wanachuoni ni kula nyama zao ilihali ni maiti na zilizo na sumu. Hili ni kutokana na madhara makubwa yanayopatikana kwa kufanya hivo.

Hivyo basi, usishangazwe unapomsikia mtu anawatukana wanachuoni. Huyu hapa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliambiwa yakuambiwa. Kuwa ni mwenye subira na huku ukitarajia malipo kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall). Atambue kuwa mwisho mwema ni wale wenye kumcha Allaah. Maadamu mtu yuko katika kumcha Allaah na yumo juu ya nuru ya Allaah, basi atambue kuwa mwisho mwema ni wa kwake.

[1] Dhul-Khuwaysirah kumtuhumu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa si mwadilifu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/256)
  • Imechapishwa: 08/03/2023