02. Hadiyth “Pindi atapojitwahirisha mtu kisha akaenda msikitini… “

298 – ´Uqbah bin ´Aamir (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

إذا تطهَّر الرجلُ، ثم أتى المسجد يَرعى الصلاة، كتبَ له كاتباهُ أو كاتبُه بكلِّ خُطوةٍ يخطوها إلى المسجد عشرَ حسناتٍ، والقاعدُ يَرعى الصلاةَ كالقانتِ، ويُكتبُ من المصلين، من حين يخرُجُ من بيتِهِ حتى يرجعَ إليه

“Pindi atapojitwahirisha mtu kisha akaenda msikitini kwa ajili ya kuswali, basi wanamwandikia waandishi wake – au mwandishi wake – thawabu kumi kwa kila hatua anayopiga kuelekea msikitini. Mwenye kukaa akisubiri swalah ni kama mswaliji; anaandikwa kuwa miongoni mwa waswaliji, kuanzia anapotoka nyumbani kwake mpaka atakaporejea.”[1]

Ameipokea Ahmad, Abu Ya´laa, at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” na “al-Ma´jum al-Awsatw”, Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake maeneo mawili.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/240)
  • Imechapishwa: 02/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy