03. Hadiyth “Mwenye kwenda msikitini kuswali mkusanyiko… “

299 – ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

مَن راحٍ إلى مسجد الجماعة؛ فخُطوةٌ تمحو سيئةً، وخُطوةٌ تكتبُ له حسنةً، ذاهباً وراجعاً

“Mwenye kwenda msikitini kuswali mkusanyiko, kila hatua anafutiwa dhambi na kila hatua anaandikiwa tendo jema – kwenda na kurudi.”[1]

Ameipokea Ahmad kwa cheni ya wapokezi nzuri, at-Twabaraaniy na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake.

[1] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/241)
  • Imechapishwa: 02/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy