02. Hadiyth “Kuna mwanamke mweusi alikuwa akisafisha msikiti akafariki usiku… “

277 – Ibn Maajah na Ibn Khuzaymah wamepokea kutoka kwa Abu Sa´iyd ambaye amesema:

كانت سَوداءُ تَقُمُّ المسجدَ، فتُوفِّيتْ ليلاً، فلما أصبحَ رسولُ الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ – أُخبِرَ بها. فقال: “ألا آذنتموني؟ “

فخرج بأصحابه فوقف على قبرها، فكبَّر عليها والناسُ خلفهُ، ودعا لها، ثم انصرف

“Kuna mwanamke mweusi alikuwa akisafisha msikiti akafariki usiku. Ilipofika asubuhi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akapata khabari juu yake ambapo akasema: “Basi ni kwa nini hamkunijuza?” Akatoka yeye na Maswahabah zake, akasimama mbele ya kaburi lake, akampigia Takbiyr na huku watu wakiwa nyuma yake na akamwombea du´aa. Kisha akaondoka zake.”[1]

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/230)
  • Imechapishwa: 24/10/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy