01. Hadiyth “Kuna mwanamke mweusi alikuwa akisafisha msikiti… “

276 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

أنّ امرأةً سوداء كانت تَقُمُّ المسْجد، ففقدها رسولُ الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ -، فسأل عنها بعد أيام، فقيل له: إنّها ماتت. فقال: “فهلا آذنتُمُوني؟ ” فأتى قبرها، فصلّى عليها.

“Kuna mwanamke mweusi alikuwa akisafisha msikiti. Baada ya masiku kadhaa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamkosa na akamuulizia. Akaambiwa kuwa amekufa. Ndipo akasema: “Basi ni kwa nini hamkunijuza?” Akaliendelea kaburi lake na kuswalia.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na Ibn Maajah kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Tamko ni lake. Imekuja kwa Ibn Khuzaymah:

إنّ امرأةً كانت تَلْتَقِط الخِرَقَ والعِيدانَ مِن المسجد

“Kuna mwanamke alikuwa akisafisha  vitambaa na vijiti msikitini.”[2]

[1] Swahiyh.

[2] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/230)
  • Imechapishwa: 24/10/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy