07. Hadiyth “Miongoni mwa matendo na mambo mema yanayomwandama muumini baada ya kufa kwake… “

275 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

إنّ مما يَلْحَقُ المؤمنَ من عمله وحسناتِه بعد موتِه، علماً علَّمه ونَشَرَه، أو ولداً صالحاً تركه، أو مصحفاً ورَّثه، أو مسجداً بناه، أو بيتاً لابنِ السبيلِ بناه، أو نهراً أجراه، أو صدقةً أخرجها من مالِهِ، في صحتِه وحياتِه، تلحقُه من بعد موتِه

“Miongoni mwa matendo na mambo mema yanayomwandama muumini baada ya kufa kwake ni elimu aliyoifunza na akaisambaza, mtoto mwema aliyemwacha, Mushaf aliyourithisha, msikiti aliyojenga, nyumba ya wapita njia aliyojenga, mto aliyochimba au swadaqah aliyotoa kutoka katika mali yake kipindi cha uzima na uhai wake – vinamfuata baada ya kufa kwake.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah, na tamko ni lake, Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” na al-Bayhaqiy. Cheni ya wapokezi ya Ibn Maajah ni nzuri.

[1] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/229)
  • Imechapishwa: 24/10/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy