03. Hadiyth “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametuamrisha kufanya misikiti… “

278 – Samurah bin Jundub (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

أمرنا رسولُ الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ – أنْ نتَّخِذ المساجد في دِيارنا، وأمَرنا أنْ نُنَظِّفها

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametuamrisha kufanya misikiti makwetu na akatuamrisha kuisafisha.” [1]

Ameipokea Ahmad na at-Tirmidhiy aliyesema:

“Hadiyth ni Swahiyh.”[2]

[1] Swahiyh kupitia zingine.

[2] Sijaiona kwa at-Tirmidhiy. Hata hivyo Abu Daawuud amepokea Hadiyth mfano wake. Imetajwa katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (481).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/231)
  • Imechapishwa: 25/10/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy