Zawadi ya kisomo cha Qur-aan ni kitu hakina msingi

Swali: Je, inafaa kusoma Suurah ndani ya Qur-aan kwa nia thawabu zake zimwendee maiti?

Jibu: Haikupokelewa katika Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yanayofahamisha kusuniwa kumpa maiti zawadi ya kisomo cha Qur-aan kama wale wanaosoma al-Faatihah juu ya roho ya maiti. Ni kitu hakina msingi. Soma Qur-aan kisha jiombee du´aa kwa Allaah na ndugu yako muislamu. Kuhusu kumpa maiti thawabu za kisomo ni kitu hakikupokelewa kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/هل-يجوز-قراءة-السورة-من-القرآن-بنية-أن-يكون-أجره-للميت-؟
  • Imechapishwa: 11/06/2022