Du´aa ya kufungulia swalah wakati imamu amerukuu au amesujudu

Swali: Wakati mswaliji anajiunga na swalah baada ya kupitwa sehemu ya swalah aombe du´aa ya kufungulia? Je, kuna tofauti kati ya Rukuu´ na hali nyingine?

Jibu: Hali inatofautiana kutegemea na ile hali ya huyo ambaye amekuja kuchelewa. Ikiwa amepitwa tu na ile Takbiyr ya kwanza na ana uwezo wa kukusanya kati ya du´aa ya kufungulia swalah na kisomo cha al-Faatihah afanye hivo. Vinginevyo atatosheka na kile kinachomuwezekea katika kusoma al-Faatihah. Kwa hayo litafahamika jibu kwa yaliyobaki. Kwa kufupisha ni kwamba amfuate imamu. Asisimame huku anaomba du´aa ilihali imamu amekwishasujudu au amekwisharukuu. Bali asujudu au kurukuu pamoja naye.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 149
  • Imechapishwa: 03/07/2022