Swali: Ni ipi hukumu ya Kiislamu kuhusu kuyatembelea makaburi na kuyafanyia Tawassul makaburi na kuchukua kondoo na mali kwa ajili ya kuyafanyia Tawassul kama vile kumtembelea bwana al-Badawiy, al-Husayn na bibi Zaynab?

Jibu: Kuna aina mbili za matembezi kuyatembelea makaburi:

1 – Aina ambayo inakubalika katika Shari´ah kwa ajili ya kuwaombea du´aa wafu, kuwaombea rehema na kwa ajili ya kukumbuka kifo na kujiandaa kwa ajili ya Aakhirah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yatembeleeni makaburi. Kwani hakika yanakukumbusheni Aakhirah.”[1]

Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiyatembelea. Vivyo hivyo Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum). Aina hii ni kwa wanamme peke yao na si wanawake. Wanawake haikusuniwa kwao kuyatembelea makaburi. Bali ni lazima kwao kuwakataza juu ya hilo. Kwa sababu imethibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi. Isitoshe kitendo cha wao kuyatembelea makaburi kunaweza kupelekea wao wakafitinisha wengine au wao wakafitinishwa, uchache wa subira na wingi wa mahuzuniko yanayowatawala.

Vilevile haikusuniwa kwao kuyasindikiza majeneza kwenda makaburi. Imethibiti katika “as-Swahiyh” kupitia kwa Umm ´Atwiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye amesema:

“Tumekatazwa kufuata jeneza na wala hatukutiliwa mkazo.”[2]

Hiyo ikafahamisha kwamba wanawake wamekatazwa kuyafuata majeneza kwenda makaburini. Kwa sababu kunachelea juu yao wakafitinisha wengine au wao wakafitinishwa na uchache wa subira. Msingi wa makatazo yanapelekea katika uharamu. Allaah (Subhaanah) amesema:

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا

”Kile alichokupeni Mtume basi kichukueni na kile alichokukatazeni basi kiacheni.”[3]

Kuhusu kumswalia maiti ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa wanamme na wanawake. Zimesihi Hadiyth kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kutoka kwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) juu ya jambo hilo. Kuhusu maneno ya ´Umm ´Atwiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa):

“… na wala hatukutiliwa mkazo.”

hayafahamishi kuwa inafaa kwa wanawake kusindikiza jeneza. Kwa sababu kule kutoka makatazo kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kunatosheleza kukatazwa. Maneno yake aliposema:

“… na wala hatukutiliwa mkazo.”

yanatokana na kujitahidi na kudhani kwake. Ijtihaad yake haifanyi kupingana na Sunnah.

2 – Aina ya kizushi. Ni pale ambapo mtu atayatembelea makaburi kwa ajili ya kuwaomba watu wake, kuwataka msaada, kuwachinjia na kuwawekea nadhiri. Mambo haya ni maovu na shirki kubwa. Tunamuomba Allaah usalama. Linaambatanishwa na hayo pale ambapo mtu atayatembelea kuwaomba du´aa, kuswali na kusoma mbele yake. Kitendo hichi ni Bid´ah na ni njia inayopelekea katika shirki. Kwa hiyo ukweli wa mambo ni kwamba zimekuwa aina tatu:

1 – Matembezi yanayokubalika katika Shari´ah. Ni pale atapoyatembelea kwa ajili ya kuwaombea du´aa watu wake au kwa ajili ya kukumbuka Aakhirah.

2 – Kuyatembelea kwa ajili ya kusoma, kuswali au kuchinja karibu nayo. Hii ni Bid´ah na ni njia inayopelekea katika shirki.

3 – Kuyatembelea kwa ajili ya kumchinjia, kujikurubisha kwake, kumwomba maiti badala yake Allaah. Au kuomba ukozi, msaada na nusura kutoka kwake. Hii ni shirki. Tunamwomba Allaah usalama.

Ni lazima kutahadhari na matembezi haya yaliyozuliwa. Hapana tofauti kati ya yule mwombwaji ni Mtume, mja mwema au wengineo. Kunaingia katika hayo yale yanayofanywa na baadhi ya wajinga pindi wanapoomba du´aa na msaada katika kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), karibu na kaburi la al-Husayn, al-Badawiy, Shaykh ´Abdul-Qaadir al-Jaylaaniy au wengineo. Allaah ndiye Mwenye kutakwa msaada.

[1] Muslim (976).

[2] al-Bukhaariy (1278) na Muslim (938).

[3] 59:07

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr min Fitnat-il-Qubuur, uk. 113-116
  • Imechapishwa: 18/07/2022