Swali: Je, inafaa kutoa Zakaat-ul-Fitwr pesa?

Jibu: Hapana. Zakaat-ul-Fitwr ni ile aliyosimulia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alifaradhisha kutoa pishi ya tende au pishi ya shayiri kuwa ni Zakaat-ul-Fitwr iliyowajibika kwa waislamu wote; mtumwa na aliye huru, mwanamume, mwanamke, mtoto mdogo na mzee na kwamba itolewe kabla ya watu kwenda kuswali.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amelengesha vitu hivi na akalengesha kiwango chake ambacho ni pishi. Visipopatikana vitu aina hii basi mtu atatoa kile chakula kinacholiwa sana na watu wa mji huo. Atatakiwa kutoa pishi na itatosha. Maneno yake  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):

“Pishi ya chakula… “

yanajumuisha kila ambacho ni chakula cha watu.

Kuhusu kutoa pesa haisihi kama Zakaat-ul-Fitwr. Mafukara siku ya ´iyd wanahitaji chakula na si pesa. Hakuna maduka yaliyofunguliwa ambapo watanunua chakula kwa pesa hizi ilihali wanataka kupika katika siku hii na wale. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ameamrisha kutoa pesa kutokana na mnasaba wa siku hii kwa sababu ni siku ya ´iyd na ni siku ya kula na kunywa. Wape chakula wafurahi na wapike na watu wengine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 28/04/2023