Swali: Je, imethibiti kuwa ´Umar aliona kuwa adhaana ya ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kuwa ni Bid´ah?

Jibu: Hapana. ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anh) ni khaliyfah wa tatu miongoni mwa makhaliyfah waongofu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Jilazimieni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu na wenye kuongoza baada yangu.”

Wanaosema kuwa adhaana ya kwanza ni Bid´ah watu hawa hawajui Bid´ah nini. Kila kitu wasichokijua wanakiona kuwa ni Bid´ah. Wanamzingatia ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) kuwa ni mzushi! Wanawazingatia makhaliyfah waongofu wazushi?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 28/04/2023