Karata na zawadi kwa mshindi

Swali: Ni ipi hukumu ya karata na wanapewa zawadi kwa mshindi kutoka kwa mtu asiyecheza na wao?

Jibu: Haijuzu. Ikiwa wanacheza kwa zawadi ni haramu kwa sababu ni kamari. Zawadi inayochukuliwa kwa ajili ya michezo ni kamari. Kuhusu kucheza karata pasi na kupokea zawadi ni haramu. Kwa sababu ni upuuzi na mchezo na ni njia inayopelekea kupokea zawadi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 28/04/2023