Swali: Ni ipi hukumu ya kumpa zakaah mtu aende kuhiji?

Jibu: Ni vizuri. Kumsaidia mtu kwenda kuhiji ni jambo zuri. Inafaa kumpa zakaah ili mtu aende kuhiji. Kwa sababu hajj ni katika jihaad katika njia ya Allaah. Miongoni mwa aina za watu wanaopewa zakaah ni pamoja na katika njia ya Allaah na hajj ni katika njia ya Allaah na ni katika jihaad. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema alipoulizwa kama inafaa kwa mwanamke kwenda kupigana jihaad ambapo akajibu:

“Ndio. Yuko na jihaad isiyokuwa na mapambano; Hajj na ´Umrah.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 28/04/2023