Zakaah ya pesa iliyowekwa benki kwa ajili ya ardhi ya biashara

Swali: Nilikusanya kiasi fulani cha pesa na kuweka benki na mwezi mmoja kabla ya kufika mwaka nilizitoa na nikanunua kipande cha ardhi kwa lengo la biashara.

Jibu: Ukinunua kwazo ardhi kwa ajili ya biashara zitahesabiwa kujengea mwaka uliopita. Kukishapita mwezi baada ya kununua kiwanja basi hesabu thamani yake na kitolee zakaah. Kwa sababu kimepitiwa na miezi kumi na mbili. Ukinunua ardhi kwa ajili ya biashara na ikapitiwa na mwezi basi itakuwa imekamilisha mwaka. Inakupasa kuitathmini kwa kushauriana na wenye uzoefu kisha baada ya hapo utaitolea zakaah ile thamani yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3800/حكم-الزكاة-في-الارض-المعدة-للتجارة
  • Imechapishwa: 02/06/2022