Swali: Je, inajuzu kuacha kufanya matendo kwa ajili ya Riyaa?

Jibu: Huu ni wasiwasi wa Shaytwaan. Nilipendelea kugusia hili lakini nilisahau. Baadhi ya watu wanaacha kufanya matendo mema; kusimama kisimamo cha usiku, wanafikia mpaka kuacha Swalah ya Jamaa´ah kwa hoja eti wanaogopa Riyaa. Hili linatokamana na Shaytwaan. Fanya matendo mema na mtakasie nia Allaah (´Azza wa Jalla) na omba kinga dhidi ya Shaytwaan. Ama kuacha matendo mema kwa kuchelea Riyaa… Kuna Athar inayosema:

“Kufanya matendo kwa ajili ya watu ni Shirki. Na kuacha kufanya matendo kwa ajili ya watu pia ni Shirki.”

Fanya matendo mema na omba kinga kwa Allaah kutokamana na Shaytwaan alofukuzwa.

Baadhi ya watu hawataki kutoa Swadaqah kwa kuogopa watu wasimtuhumu na Riyaa na unafiki. Haya yanatokamana na Shaytwaan. Achana nayo!

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_makruf%203-12-08-1433.mp3
  • Imechapishwa: 16/06/2015