Swali: Ni ipi hukumu ya kumsomea maiti Yaa Siyn kwenye kaburi? Je, Suurah hii ina fadhila?

Jibu: Yaa Siyn hasomewi anayetaka kukata roho. Hakuna dalili ya hilo. Kumethibiti Hadiyth ambayo ni dhaifu.

Kuhusiana na maiti, asisomewe kitu kutoka katika Qur-aan. Qur-aan haisomwi kwa maiti, si kabla wala baada ya kumaliza mazishi. Hakuna dalili juu ya hilo. Kitendo kisichokuwa na dalili inakuwa Bid´ah.

Ambaye nataka kumnufaisha maiti muislamu amuombee du´aa msamaha na rehema, amtolee swadaqah, amlipie madeni yake na mfano wa hayo. Haya ndio yanayomfaa maiti. Qur-aan wanasomewa waliohai ambao wananufaika kwayo na kuitendea kazi. Hawasomewi maiti ambao hawawezi kuifanyia kazi wala kunufaika kwayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (25) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ayatquran-26-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 20/06/2020