Swali: Nilisafiri kutoka Twaaif kwenda katika Umoja wa nchi za kiarabu. Ndege inaruka saa 14:00 na nilifika 17:30. Kulikuwa kumebaki dakika kumi au kumi na tano ifike Maghrib. Ningejumuisha swalah hapa kwenye uwanja wa ndege au ningeziswali wakati wa kufika kwa kuzingatia ya kwamba nilikuwa nachelea wakati usitoke?

Jibu: Ikiwa Dhuhr imeingia kabla ya ndege kuruka, basi unajumuisha Dhuhr na ´Aswr wakati wa Dhuhr. Ama ikiwa ndege inaruka kabla ya Dhuhr kuingia, basi unajumuisha Dhuhr na ´Aswr katika wakati wa ´Aswr wakati utapotua hata kama itapitika kabla ya ujua kuzama. Hakuna ubaya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (25) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ayatquran-26-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 20/06/2020