Kwa ajili hii naonelea kuwa wale wanaosafiri kwenda katika miji ya kikafiri kwa ajili ya utalii ni wenye kupata madhambi na kila pesa moja wanayoigharamikia kwa ajili ya safari hii ni haramu na ni kuharibu mali. Watahesabiwa kwayo siku ya Qiyaamah ambapo hawatopata sehemu ya kukwepea. Siku ambayo hawatopata isipokuwa yale waliyoyatenda. Watu hawa wanapoteza wakati wao, kuharibu mali yao na wanaziharibu tabia zao. Vivyo hivyo pengine wakawa hata na wasaidizi wao.

Linalostaajabisha ni kwamba watu hawa wanaenda katika miji ya kikafiri ambapo hawasikii hata adhaana wala mawaidha. Wanachosikia ni fujo za mayahudi na manaswara. Halafu isitoshe wanabakia huko kwa muda mrefu wakiwa wao, wake zao, watoto wao wa kiume na wa kike, jambo ambalo linapelekea katika kupatikana shari kubwa. Tunamuomba Allaah afya na usalama.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/23-24)
  • Imechapishwa: 11/01/2023