Wanachuoni wamesema kuwa ni wajibu kwa mtu kuhajiri kutoka katika mji wa kikafiri na kwenda katika mji wa Kiislamu ikiwa hawezi kuidhihirisha dini yake. Ama ikiwa anaweza kuidhihirisha dini yake na hafanyiwi vipingamizi akidhihirisha desturi za Kiislamu, katika hali hii Hijrah inakuwa imependekezwa na sio wajibu. Kujengea juu ya hilo, kusafiri kwenda katika miji ya kikafiri ni khatari kuliko kubaki ndani yake. Ikiwa ni wajibu kwa mtu kuharakisha kuhama kutoka katika mji wake wa kikafiri pale ambapo atakuwa hana uwezo wa kuidhihirisha dini yake, basi hali kadhalika ikiwa mtu ni muislamu na anaishi katika mji wa Kiislamu, basi haijuzu kwake kusafiri kwenda katika mji wa kikafiri kutokana na khatari inayopatikana katika dini yake na tabia yake. Ukiongezea juu ya hilo ni kuharibu pesa. Isitoshe hilo linafanya kuipa nguvu uchumi wa makafiri. Pamoja na kwamba sisi tumeamrishwa kuwachukia makafiri kwa kiasi na tunavyoweza. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قَاتِلُوا الَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ الْكُفَّارِ وَلْيَجِدُوا فِيكُمْ غِلْظَةً ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ

“Enyi Mlioamini! Piganeni jihaad na wale makafiri walio karibu nanyi na waukute kwenu ukali na tambueni kwamba Allaah yupamoja na wenye kumcha.” (09:123)

وَلَا يَطَئُونَ مَوْطِئًا يَغِيظُ الْكُفَّارَ وَلَا يَنَالُونَ مِنْ عَدُوٍّ نَّيْلًا إِلَّا كُتِبَ لَهُم بِهِ عَمَلٌ صَالِحٌ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ 

“… na wala hawakanyagi njia inayowaghadhibisha makafiri na wala hawawasibu maadui msiba wowote isipokuwa wanaadikiwa kwayo tendo jema. Hakika Allaah hapotezi ujira wa wafanyao wema.” (09:120)

Hii inahusu kafiri yeyote yule. Haijalishi kitu ni mamoja ikiwa ni mnaswara, myahudi, mkanamungu, ni mamoja ikiwa atajinasibisha na Uislamu au hajinasibishi na Uislamu. Kafiri ni adui wa Allaah, adui wa Qur-aan, adui wa Mtume Wake na waumini wote. Haijalishi kitu kutaka kwake kuwapaka watu mchanga wa machoni. Bado [siku zote atakuwa] ni adui wa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/21-22)
  • Imechapishwa: 11/01/2023