56. Qur-aan ni maneno ya Allaah kikweli na si mafumbo

Qur-aan sio mafumbo, kama wanavyosema Jahmiyyah na Mu´tazilah. Wanasema ni maneno ya Allaah, lakini hata hivyo yananasibishwa kwa Allaah kwa njia ya mafumbo kwa kuwa Allaah ndiye ameyaumba. Hivyo wanadai kuyanasibisha kwa Allaah ni kunasibisha kiumbe kwa Mola Wake. Wamesema uwongo kwa sababu kuna aina mbili ya unasibishaji:

1 – Kuegemeza maana kwa Allaah, kama vile maneno. Pindi maana inanasibishwa kwa Allaah ni kunasibisha sifa kwa Mwenye kusifika nayo. Maneno, usikizi, uoni, uwezo na matakwa ni kuegemeza sifa kwa mwenye kusifika nazo, kwa sababu maana hizi haziwezi kusimama peke yake bali zinakuwa kwa yule mwenye kusifika nazo.

2 – Kuegemeza vitu, kama vile nyumba ya Allaah, ngamia wa Allaah na mja wa Allaah.  Katika hali hii ni uegemezaji wa viumbe kwa Muumba Wake kwa njia ya utukufu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 68-69
  • Imechapishwa: 11/01/2023