Wazazi kuepuka kuwanunulia watoto michezo ilio na picha

Swali: Je, kuna tofauti baina ya watoto kutengeneza michezo hiyo na sisi kuwatengenezea au kuwanunulia?

Jibu: Mimi naona kuwatengenezea michezo kwa njia inayofanana na uumbaji wa Allaah ni haramu. Kwa sababu kitendo hichi ni katika picha ambayo hapana shaka juu ya uharamu wake. Lakini vikitujia kutoka kwa manaswara au wengine wasiokuwa waislamu basi kuwa navyo ni kama nilivyosema mara ya kwanza.

Lakini kuhusiana na kununua ni wajibu kwetu kuwanunulia vitu visivyokuwa na picha. Mfano wa vitu hivyo ni ngazi, magari na yale magari ya kunyanyua vitu.

Ama kuhusu masuala ya pamba na kitu ambacho haibaini kuwa ni picha kwa njia ya kwamba kuna viungo vya mwili kama vile kichwa na shingo, lakini hata hivyo hakuna macho wala pua, hakuna neno. Kwa kuwa haya hayapingani na uumbaji wa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/278)
  • Imechapishwa: 02/07/2017