Hukumu ya michezo ilio na vichwa vya watu au wanyama

Swali: Ni ipi hukumu ya michezo inayofanana na vichwa hivi inayotengenezwa kwa udongo kisha inabomolewa papo hapo?

Jibu: Kila anayetengeneza kitu kinachofanana na uumbaji wa Allaah kinaingia katika Hadiyth. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani watengeneza picha na kusema:

“Watu wataokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah ni watengeneza picha.”

Lakini kama nilivyosema ya kwamba ikiwa picha haiko wazi au kwa msemo mwingine haina jicho, pua, kinywa wala vidole basi hii sio picha kamilifu na wala haifanani na uumbaji wa Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/279)
  • Imechapishwa: 02/07/2017