Swali: Ulisema katika fatwa iliyotangulia[1]:

“Mwanafunzi akipewa mtihani na akawa analazimika kuchora basi achore mnyama asiyekuwa na kichwa.”

Lakini mwalimu anaweza kumfelisha mwanafunzi ikiwa hatochora kichwa. Afanye nini katika hali hiyo?

Jibu: Mambo yakiwa hivi basi mwanafunzi atakuwa amelazimishwa jambo hili na dhambi zinakuwa juu ya yule aliyemlazimisha na kumtenza nguvu. Lakini mimi nawaomba wahusika wasilikuze jambo mpaka katika hiyo ngazi  na wakawalazimisha waja wa Allaah katika kumuasi Allaah.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/masomo-yanawataka-wanafunzi-wachore-viumbe-vyenye-roho/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/274)
  • Imechapishwa: 02/07/2017