Watu watapimwa na matendo yao siku ya Qiyaamah?

Swali: Watu siku ya Qiyaamah yatapimwa matendo yao au pia watu wenyewe?

Jibu: Yatapimwa matendo na mtu mwenyewe. Amesema (Ta´ala):

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ وَلِقَائِهِ فَحَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَلَا نُقِيمُ لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَزْنًا

“Hao ni wale waliozikanusha alama za Mola wao na [pia wakakanusha] kukutana Naye basi matendo yao yameporomoka; hivyo hatutowapimia Siku ya Qiyaamah uzito wowote.”[1]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika siku ya Qiyaamah ataletwa mtu mkubwa na mnene na hatokuwa na uzito mbele ya Allaah sawa na ubawa wa mbu.”[2]

Swali: Vipi kuhusu makafiri, washirikina na wanafiki wenye unafiki mkubwa?

Jibu: Shaykh Taqiyy-ud-Diyn [Ibn Taymiyyah] (Rahimahu Allaah) amesema kuwa makafiri hawana hesabu[3]. Bali yatakusanywa matendo yao, kudhibitiwa na kuonyeshwa nayo ili wajue uovu wa matendo yao. Baada ya hapo wataingizwa Motoni, kama ilivyokuja katika maneno Yake (Ta´ala):

وَقَدِمْنَا إِلَىٰ مَا عَمِلُوا مِنْ عَمَلٍ فَجَعَلْنَاهُ هَبَاءً مَّنثُورًا

”Tutayaendea yale waliyoyatenda katika matendo, Tutayafanya kuwa ni vumbi lililotawanyika.”[4]

[1] 18:105

[2] al-Bukhaariy (4729) na Muslim (2785).

[3] Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Kuhusu makafiri, hawatohesabiwa hesabu kwa njia hiyo hiyo ya matendo mema na mabaya kupimwa, kwa kuwa hawana mema yoyote. Badala yake matendo yao yatahesabiwa na watakuja kujua hilo, wayakubali na wawajibike nayo.” (al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah)

[4] 25:23

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23355/هل-توزن-الاعمال-والاشخاص-يوم-القيامة
  • Imechapishwa: 02/01/2024