Madhambi pekee ndio yanayosamehewa

Swali: Madhambi madogo pekee ndio yanayosamehewa?

Jibu: Msingi ni kwamba kunasamehewa madhambi madogo pekee:

“… midhali mtu atajiepusha na madhambi makubwa.”

Ni sharti mtu ajiepushe na madhambi makubwa. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا

“Mkijiepusha madhambi makubwa mnayokatazwa Tutakufutieni madhambi yenu madogo na Tutakuingizeni katika mahali patukufu.”[1]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah tano, ijumaa moja mpaka nyingine na Ramadhaan mpaka Ramadhaan nyingine ni vyenye kufuta yaliyo kati yake midhali mtu atajiepusha na madhambi makubwa.”[2]

Ikiwa mambo haya makubwa ambayo ni katika nguzo za Uislamu yanafuta makosa pale ambapo mtu anajiepusha na madhambi makubwa, basi makosa mengine ni aula zaidi.

Swali: Baadhi ya watu wanakaa katika vikao wakisengenya na kufanya umbea kisha wanaambiana kuwa waseme kafara ya kikao[3] ili…

Jibu: Kwa hali yoyote kunatarajiwa kheri – Allaah akitaka.

[1] 04:31

[2] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (994).

[3] Tazama https://firqatunnajia.com/85-kafara-ya-kikao/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23360/هل-تكفير-السيىات-يكون-للصغاىر-فقط
  • Imechapishwa: 02/01/2024