13. Hadiyth ”Hakuna mja ambaye atakuswalia swalah mara moja… “

13 – ´Aliy bin ´Abdillaah ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa Ya´quub bin Zayd bin Twalhah at-Taymiy, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

أتاني آت من ربي فقال لي ما من عبد يصلي عليك صلاة إلا صلى اللهعليه بها عشرا .. فقام إليه رجل فقال : يارسول الله ألا أجعل نصف دعائيلك . قال إن شئت . قال ألا أجعل ثلثي دعائي لك . قال إن شئت. قالألا جعل دعائي لك كله .قال (( إذن يكفيك الله هم الدنيا وهم الآخرة))

”Amenijia mwenye kuja kutoka kwa Mola wangu na kusema: ”Hakuna mja ambaye atakuswalia swalah mara moja, isipokuwa Allaah atamswalia kwayo mara kumi.” Akasimama bwana mmoja na kusema: ”Ee Mtume wa Allaah! Je, nifanye nusu ya du´aa zangu ni kwako?” Akasema: ”Ukitaka.” Akauliza tena: ”Je, nifanye theluthi ya du´aa zangu ni kwako?” Akasema: ”Ukitaka.” Akauliza: ”Nifanye du´aa yangu yote kwako?” Akasema: ”Basi Allaah atakutosheleza na masononeko ya dunia na Aakhirah.”[1]

Shaykh mmoja, kwa jina Maniy´, Makkah alimuuliza Sufyaan: ”Amesikia kutoka kwa nani?” Akasema: ”Sijui.”

[1] Cheni ya wapokezi wake ni swahiyh hata kama kuna Swahabah anayekosa. Inatiwa nguvu na Hadiyth inayofuata.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 30-31
  • Imechapishwa: 02/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy