12. Hadiyth ”Yule mwenye kumswalia Mtume… “

12 – ´Abdur-Rahmaan bin Waaqid al-´Attwaar ametuhadithia: Hushaym ametuhadithia: al-´Awwaam bin Hawshab ametuhadithia: Bwana mmoja kutoka Banuu Asad amenihadithia, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin ´Amr, ambaye amesema:

من صلى على النبي صلى الله عليه وسلم كتب [الله] له عشر حسنات، ومحا عنه عشر سيئات، ورفع له عشر درجات

”Yule mwenye kumswalia Mtume, basi Allaah atamwandikia mema kumi, atamfutia makosa kumi na atamnyanyua ngazi kumi.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi wake ni dhaifu. Hata hivyo inatiliwa nguvu kupitia kwa Anas, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hadiyth hiyo ameipokea an-Nasaa´iy na wengineo kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 30
  • Imechapishwa: 02/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy