Wasia wa kuzikwa miji mitakatifu

Swali: Kuna ambaye anaacha anausia kwamba aswaliwe Makkah au al-Madiynah au azikwe kwenye makaburi yayo. Ni ipi hukumu ya wasia kama huu? Je, ni lazima kuutekeleza?

Jibu: Wasia huu si lazima kuutekeleza. Lakini ikiwepesika kuutekeleza hakuna neno. Ni jambo linaloruhusu kukiwepesika. Lakini hata hivyo si lazima.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (15) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-24-11-1434_0.mp3
  • Imechapishwa: 23/08/2019