Kukariri hajj kila mwaka au kuwaachia nafasi wengine?

Swali: Baadhi ya watu wanamnasihi ambaye kishahiji basi asihiji mara ya pili na mara ya tatu kwa hoja kwamba awaachie wengine nafasi. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Mimi nanyamaza juu ya hili. Wakati fulani tunasema kwamba tukiona msongamano mkubwa na kwamba mtu anaichokesha nafsi yake kwa jambo ambalo pengine kubaki katika mji wake akawa ni mwenye unyenyekevu na ni mwenye kumcha Allaah zaidi. Kwa sababu katika mji wake atamdhukuru Allaah, atasema “Allaahu Akbar”, atasoma Qur-aan, kufunga, kutoa swadaqah, kufanya wema na atafanya ´ibaadah zake katika hali ya utulivu. Wakati fulani tunasema kuwa hili ndio bora zaidi. Na wakati mwingine tukiona dalili zinazoshaji´isha juu ya hajj na kubainisha fadhilah zake, tunasema kuwa kufanya hajj ndio bora zaidi. Jengine ni kwamba tukiona kwamba wapo mahujaji ambao wanahiji hajj ya faradhi na wengine wanahiji hajj iliyopendekezwa. Hapana shaka kwamab zile sehemu na nembo za kufanyia ´ibaadah ya hajj kwa yule anayefanya hajj ya faradhi ndio bora zaidi. Kwani mtu huyu ndiye ana haki zaidi na sehemu hiyo kuliko ambaye anafanya hajj iliyopendekezwa tu. Mimi ni mwenye mashaka juu ya hili; nachelea nikapata dhambi kubwa nikisema mtu asifanye hajj ilihali dalili zimekuja zikihimiza juu ya hajj. Upande mwingine tukitazama manufaa na kuzuia madhara na kuwapunguzia madhara watu, pengine tukasema kuwa kuacha kufanya hajj ndio bora zaidi. Yule ambaye Allaah amemfungulia mali basi milango ya kheri iko mingi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (53) http://binothaimeen.net/content/1213
  • Imechapishwa: 23/08/2019