Wanyama ni bora kuliko waislamu watenda madhambi?

Swali: Je, mtu anaweza kusema kuwa wanyama na viumbe visivyokuwa na uhai ni bora mbele ya Allaah kuliko waislamu watenda madhambi?

Jibu: Hapana, hilo halina dalili. Ni maneno yasiyokuwa na msingi. Waislamu watenda madhambi wako na Tawhiyd na imani. Wako na msingi unaowafanya kuingia Peponi ijapo wanaweza kuanza kuadhibiwa. Wako na msingi wa Tawhiyd. Hata hivyo wamezidhulumu nafsi zao. Allaah (Ta´ala):

فَمِنْهُمْ ظَالِمٌ لِّنَفْسِهِ

“Miongoni mwao ni aliyedhulumu nafsi yake.”[1]

Swali: Lakini viumbe visivyokuwa na uhai ni bora kuliko makafiri?

Jibu: Hapana sahaka. Viumbe visivyokuwa na uhai ni bora kuliko makafiri.

[1] 32:35

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22677/هل-الحيوان-والجماد-افضل-من-العصاة
  • Imechapishwa: 17/07/2023