Ibn Baaz waislamu kuwataka msaada wakomunisti na wazushi dhidi ya waislamu wanaodhulumu

Swali: Yakipigana vita makundi mawili ya waislamu na kundi moja wapo likawataka msaada wakomunisti na wazushi – je, itawalazimu waislamu kuwasaidia dhidi ya hao wengine?

Jibu: Ndio:

وَإِن طَائِفَتَانِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ اقْتَتَلُوا فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا ۖ فَإِن بَغَتْ إِحْدَاهُمَا عَلَى الْأُخْرَىٰ فَقَاتِلُوا الَّتِي تَبْغِي حَتَّىٰ تَفِيءَ إِلَىٰ أَمْرِ اللَّـهِ ۚفَإِن فَاءَتْ فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا بِالْعَدْلِ وَأَقْسِطُوا ۖ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ

“Na mataifa [au makundi] mawili ya waumini yakipigana, basi suluhisheni baina yao. Lakini mojawapo likikandamiza jengine, basi lipigeni vitalile linalokandamiza mpaka lielemee kwenye amri ya Allaah. Likishaelemea, basi suluhisheni baina yao kwa uadilifu na fanyeni uadilifu. Hakika Allaah anapenda wafanyao uadilifu. Hakika si vyenginevyo waumini ni ndugu, hivyo basi suluhisheni baina ya ndugu zenu.” (49:09-10)

Asaidiwe yule mwenye haki. Anayekandamiza au aliyepinda ambaye ametoka nje ya dini katika wakomunisti au wapagani wasisaidiwe.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22682/ما-حكم-طاىفتين-لجات-احداهما-لاهل-الضلال
  • Imechapishwa: 17/07/2023