Wanazuoni wengi wanaona ulazima wa kulaza nia kila siku

Ni wajibu kulala na nia ya swawm kwa ajili ya kila siku. Hivo ndivo wanavoona jopo kubwa la wanazuoni. Kuhusu Abu Haniyfah na wenye kuona maoni yake hawaoni kuwa ni lazima kulaza nia. Wanachokusudia ni kwamba cheni za Hadiyth mbili hizo zimetiwa kasoro. Kinachopata kufahamika kutoka katika maneno ya Ibn-ul-Qayyim na mwalimu wake ni kuafikiana na Abu Haniyfah. Sababu mbili zimepelekea katika jambo hilo:

1 – Kutumia kipimo juu ya yaliyothibiti katika swawm zinazopendeza.

2 – Kisa cha ufaradhi wa kufunga siku ya ´Aashuuraa´.

Ni jambo liko wazi kwamba salama tahadhari zaidi ni mtu kufuata maoni ya kikosi kikubwa cha wanazuoni. Swawm ya ´Aashuuraa´ ilianza kwa kupendekezwa, kisha ikafaradhishwa, kisha ikapendekezwa tena.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/186)
  • Imechapishwa: 13/03/2024