Mmeniuliza swali hilo takiban miaka mitatu Iliyopita na nikawajibu kuwa sijasema kauli ya kukata ya kufunguza au kutofunguza. Mpaka sasa – Allaah akuhifadhi – jambo hilo limekuwa ni tatizo kwangu. Naona kuwa haitakikani kwa mfungaji kuitumia kwa sababu inafanana na vifunguzi kwa baadhi ya njia. Mfungaji aliyeniuliza kuhusu utumiwaji wake nimemkataza kufanya hivo na nikasema kuwa nachelea isije kuwa ni katika vifunguzi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/187)
  • Imechapishwa: 13/03/2024