Ameugua Ramadhaan miaka tisa hatimaye akafa

Kutoka kwa Muhammad bin Ibraahiym kwenda kwa muheshimiwa ´Abdur-Rahmaan bin Muhammad bin ´Aliy.

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته

Tumefikiwa na barua yako ambayo unauliza juu ya swawm ya mama yako na umetaja kwamba amefunga miaka tisa na maradhi yakamzidi mpaka amefikia hali ya kwamba anapoteza hisia na hawezi kuongea. Wakati mwingine akihisi nafuu anapata hisia na anaweza kuongea. Hata hivyo hakufunga Ramadhaan miaka yote hii na kwamba hatimaye akaaga dunia mwishoni mwa Sha´baan mwaka huu. Je, anapaswa kulipiwa au kutolewa chakula?

Kuhusu ule muda ambao alikuwa amepoteza fahamu swawm ni yenye kudondoka kutoka kwake. Kuhusu kile kipindi ambacho alipata nafuu, ikiwa aliweza kufunga, basi anatakiwa kutolewa chakula kwa niaba yake Mudd au nusu pishi kwa kila siku moja iliyompita kumpa masikini. Na ikiwa hakuweza kufunga mpaka akaaga dunia basi hakuna kinachomlazimu; si kumtolea chakula wala kitu kingine. Allaah ndiye mjuzi zaidi.

Muftiy wa Saudi Arabia

19/09/1385

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/185)
  • Imechapishwa: 13/03/2024