Muhammad bin Ibraahiym kuhusu swawm ya msafiri

Wanazuoni wametofautiana juu ya maoni mawili ambalo ni bora zaidi kwa msafiri. Maoni yenye nguvu ni kwamba kuacha kufunga ndio bora. Hilo ni kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hao ni waasi.”[1]

 Hao ni wale ambao hawakukubali ruhusa.

“Si katika wema kufunga safarini.”[2]

Vilevile Hadiyth ya Hamzah bin ´Amr[3].

Hili ni tofauti na swawm ya siku ya ´Aashuuraa´ ambapo Ahmad ametaja dalili ya kwamba haichukizi kwa msafiri kuifunga. Ametumia kipimo juu yake baadhi ya swawm, kukiwemo ya ´Arafah, kwa ambaye ni msafiri. Wengine wamependeza kutumia kipimo juu yake kila swawm ambayo sio ya lazima kama vile swaawm ya kufunga siku tatu kila mwezi, swawm ya jumatatu na alkhamisi na mfano wake.

[1] Muslim.

[2] al-Bukhaariy.

[3] Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/184-185)
  • Imechapishwa: 13/03/2024