Mgonjwa wa kifua kikuu cha mapafu na Ramadhaan

Swali: Kuna mgonjwa anayesumbuliwa na kifua kikuu cha mapafu na ana cheti cha daktari aliyebobea aliyemshauri kutokufunga kwa muda wa miaka mitano mfululizo. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Inafaa kukubali maneno ya daktari muislamu na mwaminifu katika mambo kama haya. Inajuzu kuchelewesha swawm kwa muda uliyotajwa kwa kufanyia kazi ushauri wake. Kuhusu daktari asiyekuwa muislamu lakini mwaminifu, pengine ikafaa kuyakubali maneno yake katika suala kama hili kwa muda wa matibabu na baada yake kwa kipindi kisichokuwa kirefu kutokana na dharurah ya kutopatikana daktari ambaye ni muislamu na mwaminifu. Hilo ni tofauti na baada ya matibabu ikiwa muda utarefuka khaswa ikiwa mtu anajihisi mwenyewe kuwa amepona kikamilifu, uchangamfu na nguvu ya kufunga na dhana yake kubwa inampelekea kwamba swawm haitomsababisha kuongezeka kwa maradhi au kuchelewa kupona.

07-02-1378

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/183-184)
  • Imechapishwa: 13/03/2024