Swali: Je, ni sahihi kumhukumu mwanamke mwenye kubaki na mume wake asiyeswali pamoja na kuwa yeye mwenyewe anajua hilo ya kwamba ni ´mzinifu`?

Jibu: Hapana. Asimhukumu. Isipokuwa ikiwa kama atahukumu hivo ni hakimu wa Kishari´ah. Kuna utata. Isitoshe haya ni masuala yenye tofauti kwa wanachuoni. Baadhi ya wanachuoni wanaonelea kuwa mwenye kuacha swalah hakufuru isipokuwa mpaka atapokanusha uwajibu wa swalah. Hahukumiwi hivi. Lakini badala yake anasihiwe mwanamke huyu asibaki. Ana haki ya kwenda kwa familia yake na kumuacha. Alazimishwe kuachana naye. Ikiwa haswali, anakunywa pombe au anafanya madhambi makubwa ana haki ya kwenda kwa familia yake ikiwa kama hakutubu. La sivyo kuombwe mtengano na atengane naye.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4743
  • Imechapishwa: 17/11/2014