Mjinga au mpotevu ndio awezae kutukana ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah

Swali: Kipindi cha mwisho kumedhihiri wanaowekea mashaka ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na wanaitukana au wanawakufurisha baadhi ya maimamu. Ni yapi maoni yako?

Jibu: Huyu anayeitukana ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ima ni mjinga na ujinga wake ndio umemfanya kufikiria hivo au ni mtu mwenye kufuata matamanio yake na mwenye ´Aqiydah potevu. Hii ndio sababu inayomfanya kuitukana ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Vinginevyo hakuna muumini anaweza kuitukana ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah anayeitakidi haki.

´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ndio ´Aqiydah ya Mitume waliyokuja nayo kutoka kwa Allaah. ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ ni yale yanayotolewa dalili na Qur-aan na Sunnah. Vipi ataweza kuitukana? Ikiwa ni Muislamu wa haki hawezi kuitukana. Lakini anafanya hivo ima ni kwa sababu ya ujinga wake. Anafikiria kuwa mwenye kufanya hivo anaenda kinyume ikiwa kama ni watu au baadhi ya watu ndio anaowatukana. Au anafanya hivo kwa sababu ya upotevu na kupinda kwake. Kwa vile ni mpotevu na ni adui wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ndio maana anawatukana.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4743
  • Imechapishwa: 17/11/2014