Swali: Kuna mtu ana janaba. Ameingia bafuni na wala hakunuia kuoga josho la janaba, bali amenuia josho ya ijumaa. Je, josho ya ijumaa inatosheleza au ni lazima arudi kuoga tena?

Jibu: Kauli sahihi ni kwamba inatosheleza. Kwa kuwa josho ya ijumaa imewekwa katika Shari´ah. Josho ya ijumaa ni wajibu kwa mujibu wa baadhi ya wanachuoni na wanachuoni wengi wanaonelea kuwa imependekezwa. Lakini hata hivyo kwa hali yoyote ile ni josho iliyowekwa katika Shari´ah. Akinuia kuoga josho ya ijumaa na janaba inatosheleza.

Ama ikiwa amesahau kuoga josho ya ijumaa lakini hata hivyo akawa ameoga kwa ajili ya kutaka kupata baridi kidogo, josho hii itakuwa haitoshelezi na wala haiondoshi hadathi. Ikiwa mtu yuko na janaba na akaoga kwa ajili ya kutaka kupata baridi kidogo – huku amesahau josho ya janaba – haitoshelezi. Ni lazima kwake kunuia kwanza kisha ndio aoge kwa ajili ya janaba. Mtume (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika ya kila kitendo kinalipwa kutegemea na nia na kila mmoja atalipwa kwa lile alilonuia.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4740
  • Imechapishwa: 17/11/2014