Kuitolea zakaah mali ya maiti aliyoacha

Swali: Thuluthi ya maiti ikifikisha mwaka wa Kiisamu (Hawl) inatolewa Zakaah?

Jibu: Hapana. Miongoni mwa masharti ya Zakaah mali iwe milki yako. Thuluthi hii sio mali yako. Maiti ameiacha itolewe katika mambo ya kheri. Ikiwa maiti ameacha thuluthi ya mali yake na ameusia itolewe katika mambo ya kheri (Swadaqah), haina Zakaah kwa sababu sio mali yako.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4740
  • Imechapishwa: 17/11/2014