Shafaa´ah kubwa ya Mtume (´alayhis-Salaam) ni kwa watu wote

Swali: Shafaa´ah kubwa ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) watu wataposimamishwa [kwa muda mrefu siku ya Qiyaamah] itakuwa kwa watu wote; waumini na makafiri au ni kwa waumini tu?

Jibu: Hapana, ni kwa watu wote. Shafaa´ah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwa watu wote; waumini na makafiri. Ni Shafaa´ah ya kutolewa watu katika kisimamo kirefu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atawaombea ili Allaah Aweze kuwatoa kwenye kisimamo kirefu hiki. Kinawahusu watu wote, Ummah wote, waumini na makafiri.

Ama kuhusu Shafaa´ah ya kuwatoa wenye madhambi makubwa Motoni, hii itakuwa maalum kwa wapwekeshaji.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4743
  • Imechapishwa: 17/11/2014