Swali: Maji yaliyopokonywa yanaondosha hadathi kubwa?

Jibu: Hili lina tofauti kwa wanachuoni. Kuna wanachuoni wanaonelea kuwa akitawadha kwa maji ya kupokonywa Wudhuu´ wake sio sahihi. Kwa ajili hii swalah yake sio sahihi. Wanachuoni wengine wanaonelea kuwa [Wudhuu´] unasihi pamoja na kwamba anapata madhambi. Anapata thawabu za swalah na anapata madhambi ya kupokonya. Ni kama mfano wa kuswali kwenye ardhi ya kupokonya au nguo ya hariri. Sahihi ni kwamba swalah yake ni sahihi pamoja na kwamba anapata madhambi. Akitawadha kwa maji ya kupokonya, akiswali kwa nguo ya kupokonya au akiswali kwenye ardhi ya kupokonya, maoni sahihi ni kwamba swalah yake ni sahihi pamoja na kuwa anapata madhambi. Ni juu yake kuleta tawbah juu ya kupokonya, kurudisha haki alichokidhulumu kwa mwenye nacho na swalah yake ni sahihi. Haya ndio maoni sahihi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4743
  • Imechapishwa: 17/11/2014