Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kwenda msikitini kwa ajili ya kuliswalia jeneza?

Jibu: Hakuna neno kufanya hivo akaenda na kuliswalia jeneza. Baada ya kufariki kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuja wanawake na wakamswalia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mmojammoja. Kila mwanamke alikuwa akimswalia kivyake kisha anaenda na kuja mwengine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (105) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/20-03-1441-H-%20igah.mp3
  • Imechapishwa: 10/10/2020