Kuoga siku ya ijumaa kunaanza wakati gani?

Ni lini kuoga josho la ijumaa kunaanza? Maoni ya karibu zaidi ya usawa yaliyosemwa ni kwamba kunaanza wakati wa kuchomoza jua. Kwa sababu baina ya kupambazuka kwa alfajiri na kuchomoza jua ni wakati wa alfajiri. Lililo salama zaidi mtu aoge baada ya jua kuchomoza. Bora mtu aoge pale atapotaka kwenda msikitini. Tukisema kuwa ni lazima kuoga, swalah ya ijumaa inasihi ikiwa mtu hakuoga? Kwa msemo mwingine mtu akikusudia kuacha kuoga na akaswali swalah yake inasihi? Jibu ni kwamba inasihi. Kwa sababu josho hili sio kwa sababu ya janaba. Ni jambo ambalo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliliwajibisha ili kubainisha sifa za kipekee za siku hii tofauti na zengine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (377) http://binothaimeen.net/content/13370
  • Imechapishwa: 10/10/2020