Wanandoa wasafiri wameamua kufungua na kujipa raha safarini

Swali: Allaah (Subnaanahu wa Ta´ala) amemuhalalishia msafiri kutokufunga. Ni ipi hukumu kwa mujibu wa Shari´ah ikiwa amesafiri na mke wake na akamjamii mchana?

Jibu: Ikiwa amesafiri umbali unaomruhusu kufupisha swalah na safari hiyo isiwe ya maasi, basi inafaa kwake kula mchana wa Ramadhaan. Qur-aan, Sunnah na maafikiano yamefahamisha hivo. Bali kikosi kikubwa cha wanazuoni wanaona kuwa funga yake ya Ramadhaan haitosihi endapo atafunga. Dalili za Qur-aan na Sunnah zinazojulisha kufaa kwa msafiri kula kutokana na safari iliyotajwa hazikutofautisha katika utumiaji wa vifunguzi kati ya kula, kunywa na kufanya tendo la ndoa. Bali inafaa kwake kuyafanya yote hayo pasi na kupambanua. Kwa msemo mwingine ni kwamba hakuna chochote kinacholazimu kutokana na haya yote yaliyotajwa katika swali.

Lipo jambo ambalo ni kwenda mbali zaidi kuliko hivo: endapo atafunga safarini kisha akafanya jimaa ndani ya swawm hiyo, atalipa funga yake tu. Hatolazimika kutoa kafara kwa sababu ya tendo lake la jimaa alilofanya, kwa sababu ni mwenye kuhukumiwa kufungua kuanzia pale alipoazimia kufanya jimaa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/196-197)
  • Imechapishwa: 19/03/2024