Kulipa deni la Ramadhaan kwa kuachanisha siku

Kutoka kwa Muhammad bin Ibraahiym kwenda kwa muheshimiwa X.

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته

Tumefikiwa na barua unayosema kuwa uko na bibi ambaye amefikisha takriban miaka 50 na kwamba alifanyiwa upasuaji mwaka wa 1386 na kwamba daktari amemkataza kufunga na kwamba hivi sasa anaelekea kupona. Anasumbuliwa na maradhi ya kisukari na hawezi kulipa swawm anazodaiwa kwa kufululiza kwa sababu anatumia dawa ya kisukari mara tatu kwa siku na mengine uliyotaja. Unauliza kama inafaa kwake kufunga kwa kuachanisha siku?

Jawabu ni kwamba hapana vibaya kulipa swawm kwa kuachanisha siku. Lakini kwa sharti kwamba asifikiwe na Ramadhaan nyingine isipokuwa awe amemaliza deni la funga yake. Jengine ni kwamba swawm, kama walivosema madaktari wenyewe, ni miongoni mwa sababu za kupunguza kiwango cha sukari.

Muftiy wa Saudi Arabia

15/06/1387

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/199-200)
  • Imechapishwa: 19/03/2024