Wakati unapokhofia busu kukupelekea katika jimaa

Swali: Ni ipi hukumu ya mfungaji anayekutana na mume wake na kumbusu pasi na kumjamii?

Jibu: ´Aaishah amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikutana katika Ramadhaan kisha akihoji: “Ni nani katika yenu ambaye anamiliki zaidi haja zake?” Umm Salamah pia ameeleza kuwa alikuwa akimbusu. Hayohayo yamesemwa pia na ´Aaishah na akaeleza:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa ni mwenye kumiliki zaidi haja zake kuwashinda.”

Je, mama wa waumini pia ni mtu mwenye kumiliki zaidi haja zake? Kinachodhihiri ni kwamba hapana vibaya kufanya hivo. Lakini akikhofia kutumbukia katika jimaa basi italazimika kwake kuepuka.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 82-83
  • Imechapishwa: 19/03/2024