Swali: Unawanasihi nini wale wanaoafikiana katika dini pasi na kusoma madhehebu fulani?

Jibu: Mwanafunzi mpya na watu wasiokuwa na elimu kubwa wanalazimika kusoma moja katika yale madhehebu manne. Ni bora kwao kufanya hivo kuliko wapotee. Hawajafikia kiwango cha wale maimamu wanne ambapo wanaweza kufanya ijtihaad zao wenyewe. Katika hali hii wanapaswa kufata kipofu. Lakini wasimfuate kipofu isipokuwa ambaye yuko na dalili kwa kile anachokisema. Yale maoni yanayoonekana kuwa na nguvu zaidi ndio wanatakiwa kuyafuata.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (30)
  • Imechapishwa: 20/02/2022