Swali: Wakati nilipokuwa nafanya Twawaaf Haram nilimwona mtu amevaa hirizi ambapo nikamvua nayo kwa nguvu. Je, nilifanya kitendo cha sawa khaswa kwa kuzingatia kwamba alikataa kuivua mwenyewe?

Jibu: Hapana, hujafanya sawa. Ulimnasihi na ukambainishia. Asiponasihika basi unatakiwa kupeleka jambo lake katika idara ya msikiti. Wao ndio wanapaswa kumvua nayo. Hakuna wanaofanya hivo isipokuwa mamlaka. Wewe unachotakiwa kufanya ni kunasihi peke yake na kubainisha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (30)
  • Imechapishwa: 20/02/2022